Aliyewai kuwa mchezaji nyota wa timu ya Chelsea, Frank Lebouef amewatupia lawama wachezaji wa Chelsea mara baada ya klabu hiyo kuwa na matokeo mabaya huku mchezo uliopita ikipoteza mchezo wa ligi kuu na kuwafanya kuwa nyuma kwa alama nane dhidi ya nafasi ya klabu nne za juu.
Mchezaji huyo wa zamani aliyekuwa akicheza kama mlinzi wa kati ambaye ni raia wa Ufaransa amesema kinachoendelea kwa sasa klabuni hapo ni kama kilichowai kutokea hapo nyuma wakati klabu hiyo ilipokuwa chini ya kocha Jose Mourinho ambapo anadai wachezaji wa Chelsea walikuwa wanacheza chini ya kiwango ili kulazimisha kocha atimuliwe, na kweli Mourinho alitimuliwa na kwa hivyo kwa sasa wanacheza chini ya kiwango ili kulazimisha klabu iachane na kocha Antonio Conte.
"Ni ukosefu wa heshima kwa mashabiki na kwa klabu, wanahusika wote katika hili kwa kocha kwa sababu tayari ameshaandaa vitu vyake na yupo tayari kuondoka lakini pia kwa wachezaji"
"Tulianza kuliona hilo kwa Mourinho, yani ni kama wachezaji wanacheza ovyo ili kuifanya klabu iharakishe kumtimua kocha haraka iwezekanavyo"
"Naijua timu inayotaka kushinda mataji na kushinda kila mchezo jinsi inavyokua uwanjani. Silioni hilo kwa Chelsea wanapokua uwanjani. Msimu uliopita unashinda ligi kuu, lakini msimu ujao unapata shida?" alisema mkongwe huyo.
Kocha Antonio Conte aliiongoza vyema Chelsea kushinda taji la ligi kuu msimu uliopita lakini sasa haionekani kuwa sawa ikishika nafasi ya tano mpaka sasa huku ikionekana kuwa na nafasi finyu ya kufudhu kucheza klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.
No comments:
Post a Comment