Asubuhi ya leo klabu ya vijana ya Chelsea ya chini ya miaka 18 imepata ushindi wake muhimu dhidi ya Southampton katika mchezo wa kombe la ligi kwa nyanda za kusini.
Magoli 4-0 yalitosha kuifanya Chelsea iondoke na ushindi huo muhimu unaowafanya kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa vijana huku ikiwa mbele kwa tofauti ya alama 12 na klabu inayoshika nafasi ya pili.
Goli la Tariq Uwakwe alilolifunga dakika ya 41 ya kipindi cha kwanza iliifanya klabu hiyo kuondoka na ushindi huo unaifanya kushinda michezo 13 mfululizo. Goli la pili la Chelsea lilifungwa dakika ya 57 likifungwa na Taylor-Crossdale wakati Anjorin akifunga jengine la tatu katika dakika ya 60 kabla ya Guehi kumaliza na kukamilisha mahesabu kwa kufunga goli la nne lililofungwa dakika ya 64, dakika nne toka kufungwa goli la tatu.
Kwa matokeo hayo, kikosi hicho kilichochini ya kocha Jody Morris kinahitaji ipate suluhu au ata kama ikipata ushindi katika mchezo ujao ambao Chelsea itakuwa uwanjani kumenyana dhidi ya West Ham.
No comments:
Post a Comment