Chanzo kimoja cha barani Ulaya kimeripoti kuwa klabu ya Chelsea inajiandaa kumtumia mlinzi wake David Luiz ili kuwanasa wawili kutoka klabu ya Napoli ya nchini Italia.
Chanzo hicho kimedai klabu ya Chelsea inakaribia kukubali mpango huo wa kumtoa David Luiz pamoja na kiasi cha pesa cha euro milioni 70 ili kuwanasa Kalidou Koulibaly pamoja na kocha Maurizio Sarri ambaye linahitajika dau la paundi milioni 8 ili kuachana na klabu hiyo.
Maurizio Sarri ambaye alikuwa kocha wa Napoli kabla ya kukataa kusaini mkataba mpya huku nafasi yake ikichukuliwa na kocha wa zanani wa Chelsea, Carlo Ancelotti anatajwa kukaribia kusaini mkataba wa kuifundisha Chelsea inayoweza kuachana na kocha wake wa sasa, Antonio Conte.
No comments:
Post a Comment