Mwanzoni ilikuwa inaitwa Chelsea Ladies lakini kwa sasa imebadili jina na kuitwa Chelsea FC Women imefanikiwa kumsainisha mkataba mpya nyota wake raia wa Norway, Maren Mjelde ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu.
Mjelde ambaye kwa sasa ana miaka 29 amefanikiwa kusaini mkataba huo leo mchana alipohojiwa mara baada ya kusaini mkataba huo alisema "Hapa (Chelsea) ni mahali pazuri na ndio maana kila mchezaji anasaini mkataba mpya"
Kocha wa kikosi hicho, Emma Hayes alipohojiwa juu ya nyota huyo kusaini alisema "Nimependezwa kwa kuona Mjelde amejidhatiti kwa kusalia klabuni hapa kwa muda mrefu"
Mjelde alisajiliwa na Chelsea mwezi Novemba mwaka 2016 na mkataba wake ulikuwa unaisha mwaka huu lakini kutokana na kusaini mkataba huo basi utamfanya kumalizana na Chelsea mwaka 2021.
No comments:
Post a Comment