Nyota na nahodha wa zamani wa Chelsea, John Terry hapo jana ameshindwa kuisaidia klabu yake anayoichezea kwasasa, klabu ya Aston Villa kufudhu kucheza ligi kuu Uingereza kwa msimu ujao mara baada ya kuruhusu kupoteza mchezo wao wa fainali waliocheza dhidi ya Fulham kwenye uwanja wa Wembley.
Aston Villa iliyoongozwa na gwiji huyo ilipoteza kwa goli 1-0 na kuzima safari ya nyota huyo aliyedumu na Chelsea kwa miaka 22 kushindwa kuisaidia klabu hiyo kufudhu kucheza ligi kuu Uingereza kwa msimu ujao.
Mchezo huo wa fainali ya klabu zilizomaliza kwenye nafasi za kucheza mtoano kwenye ligi daraja la kwanza huzihusisha zile klabu nne zilizomaliza kwenye nafasi ya tatu mpaka nafasi ya sita ambazo hucheza kwa michezo ya mtoano (play-off) ili kuzitafuta klabu mbili zitakazocheza katika fainali ambapo mshindi wa fainali hiyo ataungana na klabu mbili zilizomaliza kwenye nafasi ya kwanza pamoja na ya pili na kukamilisha klabu tatu ambazo zenyewe zinakata tiketi ya kushiriki ligi kuu.
Klabu hizo tatu ni pamoja na Wolves, Cardiff pamoja na Fulham ambao wao ndio wamefikia kwenye hatua hiyo kwa kushinda fainali ya mtoano (play-off).
John Terry ambaye kwa sasa ana miaka 37 aliungana na klabu hiyo kwenye dirisha kubwa la usajili huku akikataa ofa kadhaa za kujiunga na klabu inayoshiriki ligi kuu akikwepa kucheza dhidi ya Chelsea, klabu ambayo daima anakiri ndio klabu anayoipenda.
Lakini baadae akasema yupo tayari kucheza dhidi ya Chelsea ili kurudisha dafhila kwa mashabiki wa Aston Villa ambao walimpokea kwa furaha na wamekua wakimuonyesha upendo kwa kipindi chote.
No comments:
Post a Comment