Mmiliki wa Chelsea atoa mkono wa kwaheri kwa mashabiki wa Chelsea - Darajani 1905

Mmiliki wa Chelsea atoa mkono wa kwaheri kwa mashabiki wa Chelsea

Share This

Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich ambaye amemaliza muda wake wa kibali cha kuishi nchini Uingereza ambapo toka mwezi Aprili aliondoka nchini Uingereza na kwenda nchini kwao Urusi.

Mmiliki huyo amezua habari mpya mara baada ya gazeti la Israel kuandika habari kuwa mmiliki huyo ameanza kujenga jumba huku ikiripotiwa ana mpango wa kuhamia nchini humo.

Taarifa zilizopo zinadai mmiliki huyo anayetajwa kuwa na utajiri wa paundi bilioni 9 ameanza kujenga jumba la kifahari nchini Israel kwenye mji maarufu, mji wa Tel Aviv.

Hii inaweza kuwa dalili mbaya kwa klabu ya Chelsea ambapo kuna tetesi za mmiliki huyo kutaka kuiuza Chelsea ambapo hiyo inaweza ikalegeza matumaini ya klabu hiyo kuanza na kutekeleza upanuaji wake wa uwanja wa Stamford Bridge.

No comments:

Post a Comment