Chelsea inatajwa kuingia sokoni kumfata nyota raia wa Brazil, Malcolm Oliveira anayeichezea klabu ya Bordeaux ya nchini Ufaransa.
Chelsea inatajwa kumfukuzia nyota huyo mwenye miaka 21 ambaye alisajiliwa na klabu hiyo akitokea Corithians ya nchini Brazil miaka miwili iliyopita na tayari ameshaichezea klabu hiyo michezo 96 na kuifungia magoli 23.
Nyota huyo anatajwa pia kufukuziwa na klabu za Tottenham na Liverpool zote za Uingereza huku Chelsea ikiwa tayari kutoa paundi milioni 44 ili kumsajili nyota huyo.
No comments:
Post a Comment