Kitambo: Thibaut Courtois rasmi Chelsea - Darajani 1905

Kitambo: Thibaut Courtois rasmi Chelsea

Share This

Siku kama ya leo ya tarehe 04-Juni mwaka 2011, Chelsea ilitoa dau la euro milioni 9 kwa klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji ili kumsajili mlinda mlango wa klabu hiyo, Thibaut Courtois ambaye wakati anasajiliwa na Chelsea alikuwa na miaka 19.

Wakati anasajiliwa na Chelsea bado mlinda mlango wa kipindi iko, Petr Cech alikuwa bado kwenye ubora wake na ndipo nyota huyo raia wa Ubelgiji akatolewa kwa mkopo wa muda mrefu kwenye klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania ingawa alishasaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea Chelsea.

Alidumu na Atletico Madrid kwa misimu mitatu akiisaidia kufikia mafanikio makubwa kabla ya aliyekuwa kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kumrejesha klabuni, hiyo ilikuwa mwaka 2014.

Mwaka huohuo akasaini mkataba mpya wa kusalia klabuni Chelsea ambapo alisaini mkataba wa miaka mitano na kukabidhiwa mkataba wenye thamani ya paundi 100,000 kwa wiki ambalo hilo ni kama fungu lake la mshahara.

Mpakaa hii leo nyota huyo ameshaisaidia Chelsea kushinda mataji mawili ya ligi kuu Uingereza, taji la kombe la FA pamoja na kombe la ligi.

Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2019 ingawa Chelsea imeshajaribu mara kadhaa kujaribu kumpa mkataba mpya huku nyota huyo akisema ili asaini mkataba huo anasubiri kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia itakayofanyika uko nchini Urusi itakayoanza mwezi Juni mwaka huu.

No comments:

Post a Comment