Kona za Urusi; Chelsea kumtumia tajiri ili kumnasa shujaa wa Urusi - Darajani 1905

Kona za Urusi; Chelsea kumtumia tajiri ili kumnasa shujaa wa Urusi

Share This

Unaambiwa huko kwenye Kombe la Dunia mambo ni moto, vijana wa siku hizi wanakwambia mambo ni 'fire'. Jana kulichezwa mchezo wa kwanza ambao ni mchezo wa ufunguzi wa kundi A, Urusi ambao ni wenyeji wakiwakaribisha Saudi Arabia kwenye mchezo huo na hatimaye Urusi wakaondoka na ushindi wa magoli 5-0.

Mengi yalizungumzwa mara baada ya mchezo huo lakini kubwa zaidi lilikuwa kuhusu nyota wa mchezo huo, Aleksandr Golovin ambaye ndiye mfungaji wa goli la mwisho akifunga kwa njia ya mpigo huru (free-kick) katika dakika ya mwisho kabisa ya mchezo.

Unaambiwa tayari klabu za Man utd na Arsenal tayari washatajwa kuanza kumfukuzia nyota huyo lakini kikwazo chao kipo sehemu moja tu, kwa Chelsea maana mmiliki wa klabu yake ya CSKA Moscow ndiye anaimiliki klabu ya Chelsea namaanisha ni Roman Abramovich ambaye naye ni mrusi. Sasa kama Chelsea ikipeleka ofa tena kwa nyota huyo ambaye kabla iliwai kupeleka ofa kwake lakini Chelsea haikuonekana kuwa 'serious' sasa safari hii inaweza kutumia mgongo wa mmiliki ili kumnasa kiungo huyo mwenye miaka 22.

Lakini pia sababu nyengine inayoipa faida ni kutokana na mlinzi wa kushoto wa Urusi, Yuri Zhirkov kuwai kuichezea Chelsea kwa hiyo bado Chelsea inaweza kumtumia mlinzi huyo ili kumshawishi kiungo ambaye jana alifunga goli moja na kutoa pasi za mwisho mbili.

No comments:

Post a Comment