Chelsea inatajwa kupambana na klabu mabingwa wa ligi kuu Italia, Juventus katika vita ya kumnasa mlinzi wa klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania, Stefan Savic.
Savic mwenye miaka 27 aliwai kuichezea klabu ya Manchester city kabla ya kujiunga na klabu hiyo aliyocheza nayo kwa misimu mitatu huku akiichezea michezo 36 kwa msimu uliopita.
Chelsea inatajwa kumfukuzia nyota huyo anayecheza nafasi ya ulinzi ambaye anatakiwa pia na klabu ya Juventus.
No comments:
Post a Comment