Heri ya kuzaliwa mshambuliaji mrefu, Tore Flo - Darajani 1905

Heri ya kuzaliwa mshambuliaji mrefu, Tore Flo

Share This

Moja kati ya biashara ambazo Chelsea inajivunia kuzifanya kwenye usajili basi ni usajili wa mshambuliaji raia wa Norway, Tore Andre Flo ambaye alisajiliwa na klabu hiyo mwaka 1997 wakati Chelsea ikiongozwa na kocha mchezaji raia wa Uholanzi, Ruud Gullit.

Alitua Chelsea kwa dau la paundi 300,000 akitokea klabu ya nchini kwa Norway na kuuzwa kwa paundi milioni 12 kwenda kwenye klabu ya Rangers. Hii ni faida 40 ya dau ililotumia kumsajili mshambuliaji huyo mrefu.

Sio kwamba Chelsea ilifaidika kwenye usajili tu, hapana ilifanikiwa pia uwanjani ambapo toka amefika klabuni hapo aliifungia magoli 50 lakini pia akiisaidia Chelsea kushinda mataji manne ambayo ni kombe la FA, Ngao ya Hisani, UEFA Super Cup pamoja na kombe la washindi la barani Ulaya maarufu kama UEFA Cup Winners' Cup.

Gwiji huyo leo anatimiza miaka 45 toka kuzaliwa kwake kwenye kitongoji cha Flo huko nchini kwao nasi kama mashabiki wa Chelsea tunatumia fursa hii kumtakia kheri na fanaka kwake katika siku yake adhimu maishani.

No comments:

Post a Comment