Abramovich aifata Chelsea, afanya mkutano wa siri na Maurizio Sarri - Darajani 1905

Abramovich aifata Chelsea, afanya mkutano wa siri na Maurizio Sarri

Share This

Chelsea ilipata ushindi wake wa pili katika mchezo wake wa pili wa kirafiki mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Inter Milan kwenye mchezo wa kirafiki huko jijini Nice nchini Ufaransa.

Lakini moja kati ya mashabiki au watazamaji kwenye mchezo huo alikuwa mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich ambaye alifika jijini humo kwa ajili ya mchezo huo na ili kufanya mazungumzo na kocha mpya klabuni Chelsea, Maurizio Sarri.

Mara baada ya mchezo huo, kocha huyo raia wa Italia aliulizwa ni kipi aliongea na mmiliki huyo lakini kocha huyo akagoma kueleza.

“Ni kawaida kufanya kikao. Mambo ya kikao ni ya binafsi sidhani kama nitaeleza kipi tuliongea. Kwa hilo mtanisamehe" alisema kocha huyo.

Mmiliki wa Chelsea, Abramovich kwasasa hayupo nchini Uingereza kutokana na kibali chake cha kuishi nchini Uingereza kumalizika mwezi Aprili mwaka huu.

No comments:

Post a Comment