Bakayoko hana mpango wa kuondoka Chelsea - Darajani 1905

Bakayoko hana mpango wa kuondoka Chelsea

Share This

Gazeti la Mirror la nchini Uingereza limeripoti habari juu ya wawakilishi wa nyota wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko kueleza kwamba nyota huyo anataka kubaki klabuni Chelsea licha ya klabu kadhaa kuhitaji huduma yake.

Gazeti hilo limetoa ripoti kwamba nyota huyo raia wa Ufaransa mwenye asili ya Ivory Coast hafikirii wala kuwaza kutaka kuondoka klabuni Chelsea yenye makazi yake huko jijini London, kusini magharibi mwa nchi ya Uingereza.

Bakayoko anatakiwa kwa mkopo na klabu kadhaa ambazo ni pamoja na klabu ya Sevilla ya nchini Hispania pamoja na klabu za Inter Milan na AC Milan ambazo zote zinatoka jijini Milan huko nchini Italia zikihitaji huduma ya nyota huyo mwenye miaka 23.

No comments:

Post a Comment