Kuchelewa kwa usajili wa Higuain kutua Chelsea, sababu hii hapa - Darajani 1905

Kuchelewa kwa usajili wa Higuain kutua Chelsea, sababu hii hapa

Share This

Klabu ya Chelsea inamfukuzia mshambuliaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Argentina, Gonzalo Higuain. Lakini usajili huo umekuwa ukitajwa kwa muda mrefu, je kuna sababu gani inayofanya kuchelewa kwa usajili huo.

Moja ya waandishi wa habari huko nchini Italia aliulizwa swali kupitia mtandao wa Twitter na shabiki mmoja juu ya klabu gani itamsajili nyota huyo, ndipo nwandishi huyo akajibu akisema "AC Milan wanaonyesha nia ya dhati ya kumsajili mshambuliaji huyo lakini mchezaji huyo anataka kujiunga na Chelsea. Lakini kikwazo ni kwamba Chelsea haijaonyesha nia ya kumsajili"

Kusajiliwa kwa Cristiano Ronaldo klabuni Juventus kunatishia nafasi ya Higuain kwenye kikosi cha kwanza hivyo kuona busara kwake kuondoka klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment