Conte awacharukia viongozi wa Chelsea - Darajani 1905

Conte awacharukia viongozi wa Chelsea

Share This
Kama una kumbukumbu vyema niliwai kukuletea habari kwamba kocha wa Chelsea, Antonio Conte amewaambia marafiki zake kwamba anajiandaa kurejea klabuni Chelsea ili kujiandaa na michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya wa 2018-2019.
Licha ya kocha huyo kuhusishwa kuondoka klabuni hapo lakini bado kocha huyo anaonekana kuendelea na mkataba wake uliosalia wa mwaka mmoja ambao ameubakiza toka asaini mkataba mpya alipoisaidia klabu hiyo kushinda taji la ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2016-2017.
Kupitia gazeti la The Times limeripoti mgogoro ulioibuka klabuni Chelsea ikitaarifiwa kwamba moja ya viongozi klabuni hapo aliwatumia ujumbe (email) wachezaji wote wa Chelsea ambao hawakushiriki michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea huko nchini Urusi akiwaambia warejee klabuni siku ya jumamosi na jumapili lakini kocha huyo ametengua ujumbe huo kwa kusema yeye bado ni kocha wa Chelsea na anawaagiza wachezaji warejee siku ya jumatatu.
Taarifa hii inazidisha chumvi taarifa iliyowai kuripotiwa kwamba kocha huyo hana mahusiano mazuri na viongozi wa klabu hiyo na mtu pekee anayeongea nae ni ndugu yake aliyetoka nae nchini Italia kabla ya kufika Chelsea.
Inaelezwa kwamba wale wachezaji walioshiriki michuano hiyo na wakawai kutoka wamepewa muda wa ziada wa kurejea.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment