Kwanini Willian hajarejea klabuni Chelsea mpaka sasa? majibu haya hapa - Darajani 1905

Kwanini Willian hajarejea klabuni Chelsea mpaka sasa? majibu haya hapa

Share This

Naamini unakumbuka nilikuletea taarifa kwamba winga raia wa Brazil ambaye ni nyota wa Chelsea, Willian Borges da Silva atarejea klabuni akitokea kwenye mapumziko yake siku ya tarehe 28-Julai? unakumbuka?

Lakini baadae sikukuletea taarifa kwamba nyota huyo amesharejea klabuni au laah, lakini kiukweli hakuwa amerejea muda huo aliopangiwa kutokana na kushiriki kwake michuano ya Kombe la Dunia huko nchini Urusi.

Sasa taarifa inayoripotiwa imeeleza sababu ya nyota huyo kuchelewa haihusiani kabisa na kutakiwa na klabu za Barcelona na Man utd lakini badala yake alipewa ruhusa na uongozi wa klabu hivyo atarejea klabuni siku ya jumatano ya kesho tarehe 1-Agosti.

Nyota huyo alipoulizwa kuhusu kutakiwa na klabu nyengine hapo jana alisema ana furaha kubaki Chelsea na yupo njiani kurejea London maana kwake ni kama nyumbani.

No comments:

Post a Comment