Chelsea imekuwa ikitajwa kumfukuzia nyota wa klabu ya Napoli mwenye asili ya Brazil ingawa ni raia wa Italia, Jorginho lakini Manchester city ikaonekana inaongoza kwenye mbio za kuiwania saini ya nyota huyo mwenye miaka 27,
Hatimaye rais wa klabu hiyo ya Napoli inayoshiriki ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A, Aurelio amesema nyota huyo anakaribia kusaini mkataba wa kujiunga na Chelsea lakini akitumia nafasi hiyo ya kutangaza usajili huo kwa kuwaomba radhi Manchester city ambao walifikia hatua za mwishoni za kumnasa nyota huyo lakini inaelezwa nyota huyo alichagua kutua Chelsea kutokana na kupenda kwake kuishi jiji la London tofauti na kuishi Manchester.
Chelsea inatajwa kukubali kulipa dau la paundi milioni 51 ili kumnasa kiungo huyo pamoja na fungu la bonasi likiwa ni paundi milioni 6. Lakini katika fungu hilo kuna taarifa zinadai imejumuishwa na ela ambayo Chelsea inatakiwa kuilipa ili kumchukua Maurizzio Sarri.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment