Ramsey kuwatimua nyota wawili klabuni Chelsea - Darajani 1905

Ramsey kuwatimua nyota wawili klabuni Chelsea

Share This

Klabu ya Chelsea inatajwa kumfukuzia nyota wa klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey huku dau la paundi la milioni 30 likitajwa kuhusika kwenye usajili huo.

Ramsey ambaye ni nyota raia wa Wales amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kusalia klabuni Arsenal huku Chelsea ikitajwa kumfukuzia ili kujiweka sawa kwenye safu yake ya kiungo.

Kutua kwa Ramsey klabuni hapo kunaweza kufungua milango kwa Danny Drinkwater na Tiemoue Bakayoko kuondoka klabuni hapo ambapo Drinkwater anatakiwa na klabu za Crystal Palace, Southampton na klabu yake ya zamani ya Leicester city ambayo alikuwa akiichezea kabla ya kutua Chelsea. Bakayoko anatakiwa na klabu za Inter Milan, AC Milan na Sevilla ambazo zote zinamtaka kwa mkopo.

No comments:

Post a Comment