Kocha Maurizio Sarri atoa ufafanuzi kuhusu Ampadu na Hudson-Odoi - Darajani 1905

Kocha Maurizio Sarri atoa ufafanuzi kuhusu Ampadu na Hudson-Odoi

Share This

Chelsea imecheza mchezo wake wa pili wa kirafiki hapo jana dhidi ya Inter Milan na kufanikiwa kupata ushindi wa pili mfululizo, ushindi wa kwanza ukiwa dhidi ya Perth Glory ya huko nchini Australia.

Kwenye michezo yote hiyo imewatua makinda Ethan Ampadu na Callum Hudson ambao wote wana miaka 17.

Kutokana na kuwatumia nyota hao, kocha Maurizio Sarri ametoa majibu alipoulizwa kama makinda hao watatumika kwenye michezo ya msimu huu, haswa kwenye ligi kuu.

"Sina uhakika kama watapata nafasi ya kucheza kwenye ligi kuu, lakini naamini watakuja kuwa wachezaji wakubwa baadae" alisema kocha huyo.

Ampadu alisajiliwa na Chelsea akitokea klabu ya Exeter city ya huko nchini kwao Wales wakati Callum Hudson-Odoi akiwa ni zao la akademi ya Chelsea akiwa na mafanikio makubwa kwenye soka la ngazi ya vijana akishinda mataji na tunzo kibao.

No comments:

Post a Comment