Chelsea yaondoka na ushindi wa kanuni michuano ya ICC - Darajani 1905

Chelsea yaondoka na ushindi wa kanuni michuano ya ICC

Share This

Klabu ya Chelsea inafanikiwa kupata ushindi wake wa pili ikicheza michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya huku ikiifunga kwa njia ya mikwaju ya penati klabu ya Inter Milan.

Kipindi cha kwanza kiliisha kwa Chelsea kuongoza kwa bao 1-0, goli lililofungwa na winga, Pedro Rodriguez akimalizia shambulizi lililotengenezwa na mshambuliaji, Alvaro Morata lakini goli hilo likasawazishwa na matokeo kuwa 1-1 mpaka mchezo kuisha.

Hivyo kutokana na kanuni za michezo hii ya Kombe la mabingwa wa kimataifa (International Champions Cup-ICC) ikaamriwa mshindi apatikane kwa mikwaju ya penati ambako huko Chelsea iliondoka na ushindi wa penati 5-4.

Penati za Chelsea zilifungwa na;
Jorginho
Danny Drinkwater
Victor Moses
Tammy Abraham
Cesar Azpilicueta

Mchezo unaofata;
Chelsea vs Arsenal
Tarehe 1-Agosti
Saa 22:05 (EAT)
Aviva Stadium-Dublin

No comments:

Post a Comment