Willian aeleza tofauti ya Conte na Sarri, na mengine mengi kuhusu maisha yake klabuni Chelsea na kutakiwa na Mourinho - Darajani 1905

Willian aeleza tofauti ya Conte na Sarri, na mengine mengi kuhusu maisha yake klabuni Chelsea na kutakiwa na Mourinho

Share This
Winga nyota wa Chelsea, Willian Borges da Silva amekuwa akihusishwa kwa karibu kuondoka klabuni hapo huku akitakiwa na klabu kadhaa zikiwemo klabu za Barcelona na Manchester united huku ikiripotiwa kwamba mwenyewe ndiye analazimisha usajili huo wa kuondoka Chelsea huku sababu kubwa imekuwa ikitajwa kutokana na mahusiano ambayo hayakuwa mazuri kati yake na kocha wa zamani wa klabu hiyo, Antonio Conte.

Hatimaye nyota huyo amefanyiwa mahojiano na kuulizwa mengi yanayomhusu yeye kama mchezaji pamoja na klabu kama klabu.

Alipoulizwa anategemea nini kutoka kwa kocha wasasa wa Chelsea, Maurizio Sarri, nyota huyo raia wa Brazil alisema "Nategemea hatokuwa kama Conte (anacheka). Kufanya kazi na (Antonio) Conte ilikuwa ni kazi ngumu sana. Jinsi mitindo yake na jinsi anavyofanya mambo yake, ni kocha mgumu sana kufanya nae kazi. Unakuta unajitahidi kucheza vizuri lakini unashangazwa pale anapokufanyia mabadiliko."

"Msimu uliopita nilipotolewa niliondoka mara mbili, sikutaka kukaa kwenye benchi kwa vile sikuona haja ya kufanyiwa mabadiliko" alisema winga huyo.

Alipoulizwa kuhusu tetesi za kulazimisha kuondoka Chelsea, nyota huyo alisema "Nilimwambia kocha (Sarri) kwamba mimi sijawai kufikiria kuondoka Chelsea. Nilipata taarifa kwamba Barcelona walikuwa wananitaka. Lakini mimi kama mimi napenda nibaki hapa na nina mipango mingi nikiwa hapa. Labda klabu iamue kuniuza lakini sio mimi nitake kuondoka"

Alipoulizwa kuhusu kutakiwa na kocha Jose Mourinho kwenye klabu ya Manchester united, nyota huyo alijibu akisema "Mourinho ni kocha bora kwangu niliyewai kufundishwa nae. Ni rafiki yangu na ni mtu wa karibu kwangu huwa tunawasiliana sana na kutumiana ujumbe kupitia Whatsapp. Sina uhakika kama Man utd waliweka dau kwangu ili kunisajili lakini ningependa kuwa chini yake tena"

Kuhusu kumficha kwa vikatuni (emojis) vya makombe kocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte kwenye picha aliyotuma mtandaoni ya kushangilia ubingwa wa kombe la FA, nyota huyo alisema "Mara baada ya msimu kumalizika, nilisafiri kurejea nchini Brazil ili kujiandaa na Kombe la Dunia lakini nikiwa huko mtoto wangu alichezea simu yangu na kuziweka zile 'emojis' alipo kocha Conte. Wakati nilipochukua simu sikuangalia hilo nikajikuta nishaituma"

Hayo na mengine mengi usisahau kutufuatilia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram ambapo tunapatikana kwa jina la darajani1905 wakati Facebook tuna kurasa mbili ambazo ni Darajani 1905 na Chelsea 1905. Shukrani sana

No comments:

Post a Comment