Mpaka sasa Jorginho amepata kadi za njano 9, endapo kwenye mchezo dhidi ya Man utd akapata kadi nyengine ya njano atakosa michezo miwili ya ligi kuu dhidi ya Tottenhan na Bournemouth.
Sheria na kanuni ya ligi kuu Uingereza ipo hivi;
Ukipata kadi za njano 5 kabla ya mechi ya raundi ya 19 ya ligi kuu, utaukosa mchezo mmoja unaofata!
Ukipata kadi za njano 10 kabla ya mechi ya raundi ya 32 ya ligi kuu, utakosa michezo miwili inayofata!
Ukipata kadi za njano 15 kabla ya mechi ya raundi ya 38 ya ligi kuu, utakosa michezo mitatu inayofata kwa msimu unaokuja!
Kwa hivyo mchezo wa Chelsea dhidi ya Man utd utakuwa mchezo wa raundi ya 26, hivyo Jorginho akipata kadi ya njano atakuwa ametimiza kadi za njano 10 kabla ya mchezo wa raundi ya 32 hivyo atakumbwa na adhabu ya kukosa michezo miwili ambayo ni dhidi ya Tottenham na dhidi ya Bournemouth.
Wakati huohuo Mateo Kovacic pia ana kadi 8 za njano, naye akipata kadi 10 za njano kabla ya mchezo wa raundi ya 32 inamaana ataingia kwenye adhabu hiyo.
Jorginho na Kovacic wamekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Chelsea kilicho chini ya kocha Lampard kwenye msimu huu wa kwanza kwa kocha huyo ndani ya ligi kuu Uingereza.
No comments:
Post a Comment