Chelsea yaongoza duniani kwa kuvuna pesa ndefu, kuitumia kwenye kusajili? - Darajani 1905

Chelsea yaongoza duniani kwa kuvuna pesa ndefu, kuitumia kwenye kusajili?

Share This

Mtandao wa CIES unaotoa takwimu kuhusu maswala ya soka umeitaja Chelsea kama  klabu iliyovuna faida nyingi kwenye madirisha mawili ya usajili yaliyopita.

Chelsea ilitengeneza takribani paundi milioni 85 kwa kumuuza nyota wake, Eden Hazard ambaye alijiunga na Real Madrid uku bado ikiwa inapokea fedha kutokana na  kiwango atakachokionyesha nyota huyo klabuni huko.

Usajili huo na sajili nyengine zimeifanya Chelsea kuingiza paundi milioni 174 kwenye madirisha yote ya msimu wa 2019-2020 uku yenyewe ikitumia paundi milioni 38 kumsajili Mateo Kovacic.

Chelsea ni klabu pekee kwenye timu kumi zilizotengeneza faida kubwa kwenye madirisha hayo mawili uku klabu ya Real Madrid ikitajwa kama klabu iliyotengeneza hasara zaidi ikiwa imetumia paundi milioni 153.


Faida hiyo iliyoingiza Chelsea inaifanya kuwa klabu iliyotengeneza faida kubwa kuliko klabu yeyote duniani, sasa swali ni je, fungu hilo litatumika kwenye dirisha kubwa lijalo kusajili nyota wapya haswa ukizingatia Chelsea haijafanya usajili kwenye madirisha haya mawili ukiachana na Mateo Kovacic ambaye aliruhusiwa kusajiliwa kwa kuwa alikuwa kwa mkopo klabuni hapo toka msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment