Gilmour, rasmi apandishwa timu ya wakubwa ya Chelsea - Darajani 1905

Gilmour, rasmi apandishwa timu ya wakubwa ya Chelsea

Share This
Nyota kinda wa Chelsea, Billy Gilmour amejumuishwa kwenye timu ya wakubwa ya Chelsea akitolewa kwenye ngazi ya soka la vijana alipokuwa akiitumikia timu ya vijana ya Chelsea.


Nyota huyo raia wa Scotland amepandishwa rasmi uku ikithibitishwa na yeye mwenyewe akisema kocha Frank Lampard alimwambia likizo ya ligi kuu Uingereza ya kipindi cha baridi itakapoisha atakuwa sehemu ya timu ya wakubwa.

"Kwenye mechi ya ugenini dhidi ya Leicester, nilijumuishwa kwenye kikosi ingawa sikupata nafasi, kocha Frank Lampard aliniita na kuniambia baada ya likizo ya majira ya baridi nitakuwa sehemu ya kikosi cha wakubwa." amethibitisha kinda huyo.


Nyota huyo anayecheza nafasi ya kiungo amekuwa sehemu muhimu ya muhimili ya kikosi cha Chelsea kwa soka la vijana tangu aliposajiliwa mwaka 2017 akitokea klabu ya Rangers ya nchini kwao Scotland.

No comments:

Post a Comment