Caballero akalia kuti kavu kisa Arrizabalaga - Darajani 1905

Caballero akalia kuti kavu kisa Arrizabalaga

Share This

Kumekuwa na taarifa nyingi zikizungumzia au kuripoti nafasi ya golikipa klabuni Chelsea uku kukiwa na taarifa nyingi zinazotaarifu mwenendo mbaya wa uwezo wa kipa nambari moja, Kepa Arrizabalaga uku wakitajwa makipa kadhaa kutakiwa ili kuziba pengo la mlinda mlango huyo.

Lakini leo imechapishwa taarifa inayoleta mtazamo mpya na taswira mpya ikieleza kwamba aliyekalia kiti cha moto kwenye nafasi hiyo ni kipa namba mbili, Willy Caballero.


Taarifa hizo zinaeleza kwamba Chelsea ipo tayari kuingia sokoni kumsajili mbadala wa Caballero atakayekuja kwa lengo la kumpa changamoto Kepa Arrizabalaga uku Caballero akionyeshwa mlango wa kutokea.

Inaelezwa kwamba Chelsea inataka kumsajili kipa mwenye ushindani zaidi ili kupambania nafasi na Kepa Arrizabalaga kisha kumruhusu Caballero mwenye miaka 38 aondoke.

Mkataba wasasa wa Caballero ndani ya Chelsea unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment