Mkongwe wa soka aishauri Chelsea kumsajili nyota huyu wa Ufaransa - Darajani 1905

Mkongwe wa soka aishauri Chelsea kumsajili nyota huyu wa Ufaransa

Share This
Nyota wa zamani wa klabu ya Arsenal, Charlie Nicholas ameishauri Chelsea kuingia sokoni kumsajili nyota na mshambuliaji raia wa Ufaransa, Odsonne Edouard.


Nyota huyo mshambuliaji anayeichezea klabu ya Celtic ya nchini Scotland amekuwa kwenye kiwango kizuri akifunga magoli 24 ndani ya michezo 37 anatajwa na gwiji huyo kama angesajiliwa na Chelsea angekuwa mchezaji mzuri na tishio.

"Edouard anafaa kwenda Chelsea au Man utd, nina hakika na ninaongea kwa kujiamini kwamba angeendana vizuri na timu mojawapo."

"Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na kwa hakika sina wasiwasi na uwezo wake." amesema gwiji huyo ambaye pia aliwai kuichezea Celtic na ni raia wa Scotland, Charlie Nicholas.

Edouard alisajiliwa na Celtic mwaka 2018 akitokea PSG ya Ufaransa na mara kadhaa anapoulizwa kama anajutia kuondoka PSG anasema hapana na anajivunia kuwa Scotland.

No comments:

Post a Comment