BENTEKE AIHOFIA KOMBE LA DUNIA KUTUA CHELSEA - Darajani 1905

BENTEKE AIHOFIA KOMBE LA DUNIA KUTUA CHELSEA

Share This

Mshambuliaji wa klabu ya Crystal Palace, Christian Benteke ambaye amekuwa akitajwa kutakiwa na Chelsea amepindua usajili huo mara baada ya wakala wake kusema nyota huyo raia wa Ubelgiji kutotaka kuondoka.

Wakala wake akihojiwa kuhusu nyota huyo alisema "kabla ya kuanza kwa msimu, Benteke aliniambia hataki kuondoka Crystal kutokana na kutaka kuwa na uhakika wa kuchaguliwa kucheza kombe la dunia mwakani huko Urusi"

Kwa maelezo ya wakala huyo ameeleza kuwa kinachomfanya Benteke aendelee kusalia Crystal ili apate uhakika wa kuitwa kwenye timu ya taifa ya nchini kwao itakayosafiri kwenda kwenye michuano ya kombe la dunia mwakani ambapo kwa maana hiyo haiwezekani kwa mchezaji huyo kuondoka kipindi iki.

Ila je unazani Chelsea inamtaka mtu kama Benteke?

No comments:

Post a Comment