NYOTA WA CHELSEA WAINGIA KIKOSI BORA - Darajani 1905

NYOTA WA CHELSEA WAINGIA KIKOSI BORA

Share This
Ni raundi 18 katika ligi kuu Uingereza zishakamilika mpaka sasa ambapo imesalia raundi moja tu kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ambapo kila timu ishavuna kile ilichostahili kukivuna kutokana na ilivyojiandaa katika msimu huu wa 2017-2018.

Mpaka kufikia raundi zote hizo, chombo cha habari za michezo cha Skysports kimewachagua wachezaji bora waliounda kikosi cha pamoja kwa mjumuisho wa timu zote za ligi kuu Uingereza ambapo Chelsea kama mabingwa watetezi tumefanikiwa kuingiza wachezaji watatu kati ya 11.
Cesar Azpilicueta ambaye kati ya mechi 56 ya ligi kuu akiwa chini ya Antonio Conte amekosa mchezo mmoja tu toka msimu uliopita, huku Marcos Alonso na Hazard wakikamilisha idadi hiyo.

Hongera kwa nyota wetu, Cesar Azpilicueta, Marcos Alonso na Eden Hazard.

No comments:

Post a Comment