MOURINHO AYAZUA MENGINE HUKO - Darajani 1905

MOURINHO AYAZUA MENGINE HUKO

Share This
Achana na kile alichotufanyia sisi kwa kuwauza Kevin De Bruyne ambaye kwa sasa anang'aa huko Man city na kumuuza Mohammed Salah ambaye kwa sasa ndiyo nyota na mfungaji bora wa ligi kuu Uingereza akiwa pale Liverpool, sasa kocha Jose Mourinho ameanza kukosolewa juu ya kuuza kwake ambako huko alipo kwa sasa, Man utd inaelezwa yupo kwenye mipango ya kumuuza nyota wa klabu hiyo, Enrick Mkhitaryan. Sasa wachambuzi wa soka wamekuja juu na kuanza kumkosoa juu ya mpango wake huo.

Rafael Honigstein ambaye ni mchambuzi wa soka katika chombo cha ESPN amesema "itakuja kumsababishia makubwa baadae, ingawa inawenda yasiewe makubwa kama kwa De Bruyne na Mo Saah" akimaanisha kumuuza Mkhitaryan kunaweza kumfanya akaja akaumbuka baadae.

No comments:

Post a Comment