Mchambuzi wa soka Phil Lythell ameitahadharisha Chelsea juu ya mpango wake wa kutaka kumnunua kiungo mshambuliaji nyota wa Everton, Ross Barkley ambaye ni raia wa Uingereza.
Lythell ameitahadharisha Chelsea akiamini kuwa nyota huyo hatokuwa na nafasi Chelsea na kumnunua itakuwa sawa na kazi bure.
Amesema "Barkley anaweza kucheza kama kiungo mshambuliaji au namba 10 ambapo majukumu hayo yanatimizwa pia na Eden Hazard, lakini pia Cesc Fabregas na Willian wote wanafanya kazi hiyo"
"lakini pia kutakuwa na nafasi ya Loftus-cheek ya kurejea Chelsea, je atacheza nafasi gani wakati majukumu yake ni sawa na ya Barkley, wote wana mtindo sawa wa kucheza soka, lakini pia Barkley amekaa nje kutokana na majeruhi. Je unazani akifika Chelsea atarudi kwa haraka kwenye kiwango chake cha mwanzo?" alisema mchambuzi huyo akiitahadharisha Chelsea.
No comments:
Post a Comment