Mshambuliaji na nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye amekuwa akitajwa kama moja ya vipaji bora kuwai kutokea amejitoa kama nyota watakaokuja kushinda tunzo ya mchezaji bora maarufu kama Ballon d'or.
Hazard wakati alipohojiwa alisema "katika kubeba tunzo hiyo namuona Kylian Mbappe, anajua soka, anajua kufunga na hata kuujua mpira" alisema Hazard akimtaja nyota huyo mpya wa klabu ya PSG ambaye aliwai kutakiwa na Chelsea pindi alipokuwa AS Monaco.
"labda nitakuja kushinda tunzo hiyo lakini kwa sasa namuona Mbappe ndiye atakayeweza kuvunja ufalme wa Ronaldo na Messi" aliongezea.
Lakini pia alipoulizwa kuhusu kumuonaje mlinzi wa klabu ya Chelsea, Andreas Christensen, Hazard alijibu "nimemwangalia sana, na kwa umri kama wake alafu kucheza kwa nafasi anayocheza nadhani ana uwezo mkubwa. Nimemfahamu Christensen muda mrefu sasa toka akiwa Borrusia Monchnglebach ambapo huko alicheza na Thorgan Hazard(mdogo wa Hazard.
No comments:
Post a Comment