Nyota wa Chelsea, Eden Hazard ameamua kufunguka na kuongea juu ya anadhani Chelsea ina nafasi tena ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu Uingereza msimu huu huku Chelsea ikiwa nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu Uingereza.
"ndiyo tunaweza kubeba ila ni ngumu sana kufanya hivyo. Wakati naanza msimu nilikuwa natamani nishinde taji la ligi kuu kisha mwakani nikabebe taji la kombe la dunia. Lakini sasa naona kushinda ligi kuu ni kazi kutokana na uwezo wa Manchester city" alisema Eden Michael Hazard ambaye kiasili ni raia wa Ubelgiji.
Chelsea imeachwa alama 14 na vinara Manchester city inayoongoza msimamo wa ligi kuu ikiwa na alama 52 huku ikipoteza alama 2 tu wakati kwa upande wa Chelsea tumepoteza alama 16 kati ya michezo 18 huku ikiwa nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu.
"nachotaka kumwambia Kevin (De Bruyne) anatakiwa ashinde ligi kuu ili aje Ubelgiji akiwa na hali ya ushindi ili tubebe kombe la dunia kwa ajili ya raia wa Ubelgiji. Kevin ni rafiki yangu ingawa tukicheza dhidi ya Man city urafiki wetu huwa pale dakika 90 zinapoisha" alisema Hazard akiipa nafasi Man city anayochezea mchezaji nyota Kevin De Bruyne ambaye ni taifa moja na Hazard, wote ni wabelgiji.
No comments:
Post a Comment