Mara baada ya nyota wa Chelsea, Eden Hazard kuhusishwa na kuondoka Darajani, huku akihusishwa kutimkia Real Madrid au kwa watani zetu Manchester united huku kocha wao, Jose Mourinho akitajwa kumfukuzia kwa karibu nyota huyo huku kukiwa na taarifa kuwa watani zetu hao wapo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 90. Basi nyota hawa wanaweza wakachukua nafasi ya nyota huyo raia wa Ubelgiji.
Thomas Lemar
Nyota hyu amekwa akitajwa kwa karibu kuhusishwa na klabu ya Arsenal ila sasa Chelsea imejitosa kwa winga huyo anayeichezea klabu ya nchini Ufaransa, AS Monaco ambapo ametokea kiungo machachari wa Chelsea, Tiemoue bakayoko.
Ross Barkley
Nyota raia wa Uingereza ambaye katika dirisha kubwa la usajili lililopita alikaribia kwa karibu kutua Darajani ambapo alishafika kwenye makao ya Chelsea ili kufanyiwa vipimo kujiunga na The Blues kabla ya kughairi na kurudi zake Everton, klabu ambayo bado anaichezea mpaka sasa ivi. Anatajwa tenakutakiwa na Chelsea ambapo anaonekana labda ataweza kuziba pengo la nyota, hazard.
Leon Bailey
Ni nyota aliyewai kucheza na mtanzania, Mbwana Samatta wakiwa nchini Ubelgiji kwenye klabu ya KRC Genk ambayo pia ilishawai kutoa zao ambalo lipo Chelsea kwa sasa, Thibaut Courtois. Lakini baadae Bailey akatimkia zake Bayer Leverkusen ambapo ndipo anaichezea mpaka muda huu akiwa nyota klabuni hapo ambapo ameanza kuhusishwa kutakiwa na Chelsea kipindi hichi pia ambacho Hazard anatajwa kuondoka klabuni.
HAZARD AKIONDOKA, CHELSEA ITAWAVUTA NYOTA HAWA
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment