KOCHA ANTONIO CONTE AISHAURI CHELSEA - Darajani 1905

KOCHA ANTONIO CONTE AISHAURI CHELSEA

Share This

Chelsea inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza, huku ikiwa na alama 42 kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza ikiwa imeachwa alama 16 na vinara wa ligi hiyo, Mama site (Man city) iliyo na alama 58.

Kuelekea mchezo wa ligi kuu jumamosi hii ambapo Chelsea itashuka Stamford Bridge kumenyana na Stoke city katika mchezo wa mwisho kwa mwaka 2017 huku ikitimiza mchezo wa 21 kwenye ligi kuu, Conte ameishauri Chelsea kupambana kutafuta nafasi ya timu nne za juu kwenye ligi hiyo ambazo zitafanikiwa kufuzu kucheza ligi ya mabingwa Ulaya.

"Unapata nguvu ya kupambana kwenye ligi kuu kutokana na msukumo wa ligi ulivyo, lakini nadhani Chelsea ipambane kutafuta ligi kuu kuliko kuangalia jinsi ya kubeba ligi kuu" alisema Conte.

"Unashindana na klabu yenye ubora zaidi, Man city imekuwa bora msimu, kucheza michezo 20 huku ikipata suluhu mchezo mmoja na haijapoteza, unadhani itakuwa rahisi kumsimamisha?"

"Kilichobaki kwa sasa ni kuangalia nafasi ya kushiriki, ligi ya mabingwa Ulaya maana nafasi hiyo ipo kwa timu nne tu na nakumbuka msimu uliopita Man united na Arsenal zilimaliza chini ya klabu nne ambazo zingeweza kufuzu ligi ya mabingwa kwa hiyo sio rahisi" alisema Conte.

No comments:

Post a Comment