Aliyewai kuwa kocha wa Manyumbu (Man united) ambapo kabla alianzia Everton na kutimkia hapo Unyumbuni kisha kutokomea Hispania ambako huko alitimuliwa kutokana na kuwa na matokeo mabovu sasa yupo West Ham pale Uingereza akiiongoza klabu hiyo kupambana kutoshuka daraja, David Moyes huenda akamchukua nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea ambaye kwa sasa anaichezea Borrusia Dortmund ya Ujerumani, Andrea Schurlle.
Schrulle anasota kutafuta nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu yake ya Borrusia Dortmund huku akitaka kupata nafasi ili aonyeshe kiwango chake aweze kuitwa kwenye kikosi kitakachosafiri kwenda kumenyana nchini Urusi kwenye michuano ya kombe la dunia ambapo winga huyo anatokea timu ya Ujerumani.
Huenda Schurlle akajiunga na West Ham ambayo ndiyo inayotajwa kumuwania.
No comments:
Post a Comment