BARKLEY; NILIKATAA KUTUA CHELSEA, KWA SABABU.. - Darajani 1905

BARKLEY; NILIKATAA KUTUA CHELSEA, KWA SABABU..

Share This

Hapa nimekuletea mahojiano aliyoyafanya nyota mpya wa Chelsea, Ross Barkley juu ya kwanini alikataa kutua Chelsea katika dirisha kubwa la usajili ambapo kama unakumbuka vizuri alishafika mpaka kwenye vipimo ila baadae akaghairi.

Kwanini alikataa kutua Chelsea katika dirisha kubwa la usajili
Ross Barkley alijibu "Nilipata majeraha mabaya sana. Nilijiumiza lakini kabla ya hapo nilikuwa nishafanyiwa upasuaji wiki mbili kabla kwa hiyo kabla hata ya kuanza kwa msimu nilikuwa nishafanyiwa upasuaji mara mbili"

"Kwa kipindi kile nilikuwa nashinda hata kutembea, nilikuwa nikitembea kwa kusaidiwa na vifaa maalumu, nilikuwa nashindwa kufanya chochote kwa uwezo wangu mwenyewe kwa wiki sita. Nilifikiri haukua wakati sahihi kwangu kujiunga na klabu nyengine. Nilitaka kuwekeza akili yangu kwenye kurudia hali yangu ya kawaida ili kuweza kurudia pale nilipopanga kufikia"

"Kabla ya hapo sikuwai kupata majeraha ya msuli, ilinikuta vibaya sana hali ile. Nilipata majeraha yale nikiwa mazoezini, nilijaribu kumzuia mchezaji mwenzangu na nikasikia kama kuna kitu kimetokea ghafla kwenye mguu wangu, nilipata maumivu makali"

"Baada ya wiki mbili, nilifanyiwa upasuaji hapahapa London na ndoto zangu zikawa kama hazina mdhamana na niliwaza ungekuwa muda sahihi kuangalia nitarejea vipi kwenye hali yangu ya uzima na niliona kuja hapa ungekuwa ni usajili muhimu sana kwangu"

Kuhusu kufika Chelsea...

Ross Barkley alijibu "Nina furaha na nategemea kushinda mataji mengi nikiwa hapa, na kama inavyofahamika Chelsea ni moja ya klabu zinazoshinda mataji na kutoa changamoto kwa mataji mengi. Na hilo ndio lilikuwa lengo langu kushinda mataji tofauti tofauti na kujipa changamoto kwa kucheza dhidi ya wachezaji bora duniani"

***Je unadhani Chelsea itakuwa klabu ya kujivunia kwa Barkley?

No comments:

Post a Comment