Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa klabu ya As Roma imekubali kuwauza nyota wake Edin Dzeko na Emerson Palmieri kutua klabuni Chelsea kwa kiasi cha Euro milioni 55 ambapo usajili huo unaweza kukamilika siku ya jumatatu au jumanne ya wiki ijayo.
Taarifa zilizoliripotiwa na vyombo vya habari kadhaa kama Sky Sports Italia na Calciomercato.it vya nchini Italia vimesema dili hilo lipo karibuni kukamilika huku mgawanyo wa viwango vya pesa kwa nyota hao ukiwa kwa Edin Dzeko atanunuliwa kwa Euro milioni 30 wakati kwa Emerson akiwa na thamani ya Euro milioni 20 wakati hiyo Euro milioni 5 ikiwa ni kama nyongeza.
Wakati sababu kubwa inayotajwa kuwachelewesha nyota hao kusafiri kwenda Chelsea ili kukamilishiwa vipimo ikiwa ni mchezo wa ligi kuu Italia ambapo As Roma itacheza dhidi ya Inter Milan ambapo mara baada ya nyota hao kucheza mchezo huo ndio wanaelezwa watachukua ndege ili kutua Chelsea.
Dzeko atakayetimiza miaka 32 ufikapo mwezi Machi, alisajiliwa na As Roma mwaka 2015 akitokea Mama site (Manchester city) kwa dau la Euro milioni 15 ambapo kumuuza kwa Euro milioni 30 itakuwa ni faida kwa As Roma wakati kwa Emerson ambaye anaichezea timu ya taifa ya Italia ingawa ana asili ya Brazil alisajiliwa kutoka Santos ya Brazil kwa dau la Euro milioni 2 na leo kuuzwa kwa Euro milioni 20 itakuwa ni faida zaidi kwa As Roma.
No comments:
Post a Comment