Chelsea inatajwa kuwafukuzia nyota wawili kutoka ligi kuu Italia ambao wote wanatajwa kutokea As Roma, Emerson Palmeira na Edin Dzeko wanatajwa kutakiwa na Chelsea kabla ya kufungwa kwa dirisha hili la usajili.
Wakala wa Emerson alipoulizwa juu ya mchezaji wake kutua Chelsea alijibu kuwa mazungumzo yanaendelea kufanyika kati ya mchezaji na klabu lakini pia kati ya klabu ya Chelsea inayofanya mazungumzo na klabu ya Roma ili kumsajili mlinzi huyo raia wa Italia mwenye asili ya Brazil.
Lakini pia, Chelsea inatajwa kumfukuzia Edin Dzeko kutoka klabuni hapohapo As Roma ambapo kumtaka mshambuliaji huyo ili akawe mbadala wa Alvaro Morata pale klabuni Chelsea kutokana na mbadala wa sasa, Michy Batshuayi kuonekana bado hajawa sawa.
Chelsea ipo tayari kutoa Euro milioni 50 ili kuwasajili nyota hao wote na bado mazungumzo yanaendelea.
No comments:
Post a Comment