FIFA KUIFUNGIA CHELSEA - Darajani 1905

FIFA KUIFUNGIA CHELSEA

Share This

Shirikisho la soka duniani maarufu kama FIFA linatajwa kuikuta na hatia klabu ya Chelsea kwa kuvunja kanuni ya kufanya usajili ambapo Chelsea ilikuwa kwenye uchunguzi ikichunguzwa juu ya usajili iliyofanya kwa kuwasajili wachezaji makinda wengi tena kutoka nje ya Uingereza, uchunguzi huu ulianza toka kulipokuwa na sintofahamu ya kusajiliwa Betrand Traore ambaye ni raia wa Burkina Faso na kwa sasa anaichezea klabu ya Olympique Lyon.

Chelsea inaelezwa kufanya usajili wa wachezaji wengi ambao wengi wao walikuwa bado hawajafikisha umri wa kuwa mtu mzima yaani miaka 18 tena wakitoka nchi za mbali na kupelekwa kwenye akademi ya Chelsea.

Kutokana na kuvunja kanuni hiyo, Chelsea imepewa adhabu ya kutokusajili mchezaji yoyote aliyechini ya miaka 18 na ata kama ikimsajili basi asiwe anatoka umbali wa kilometa 50 kutoka ilipo mipaka ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment