Klabu ya Chelsea inatajwa kuachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji raia wa Ufaransa, Olivier Giroud kutoka klabuni Arsenyani (Arsenal) na inatajwa kuifukuzia saini ya nyota kutoka klabuni Tottenham, Fernando Llorente ambaye kwa sasa ana miaka 32.
Chelsea iliwai kumfukuzia mshambuliaji huyo raia wa Hispania ambaye mwishowe alikubaliana na ushawishi wa Mauricio Pochettino ambaye ni kocha wa Tottenham na kukubali kujiunga na klabu hiyo akitokea Swansea na toka amejiunga na klabu hiyo amekuwa na nafasi ndogo ya kupata nafasi huku akishindwa kumpa changamoto mshambuliaji nyota wa klabu hiyo, Harry Kane.
Kocha Antonio Conte aliwai kufanya kazi na mshambuliaji huyo raia wa Hispania pindi alipokuwa Juventus ambapo kocha Conte alikuwa kocha wa klabu hiyo kabla ya baadae kutimkia Swansea.
Chelsea inaonekana kuwa na uhitaji mkubwa wa mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga magoli ya vichwa ambapo imehusishwa na nyota kama Andy Carroll, Peter Crouch, Edin Dzeko na hata Barnes. Na huku kukiwa na taarifa kuwa Tottenham anataka paundi milioni 25 ili imuachie mshambuliaji huyo.
No comments:
Post a Comment