Kwanza nianze kwa kukuomba samahani kwa kutokuletea kilichojiri katika mchezo wa jana ambapo Chelsea ilipata ushimdi wa matuta au penati katika mchezo wa hatua ya nne ambapo Chelsea ilikuwa ikishuka uwanjani kuikaribisha Norwich katikakombe la FA, ambapo mchezo huo uliisha kwa sare ya 1-1 kwa dakika za kawaida ndipo zikaongezwa dakika 30 yaani 15 za kipindi cha kwanza na 15 kipindi cha pili ambapo katika muda huo Chelsea ilicheza pungufu mara baada ya wachezaji wake wawili kuonyeshwa kadi nyekundu ambao ni Pedro na Alvaro Morata lakini Mungu akasaidia wale watoto hawakufanikiwa kutumia udhaifu wetu ndipo mpira ukatakiwa kwenda matuta mara baada ya kuisha dakika 30. Kwenye matuta kama kawaida Willy Caballero akatupatia ushindi muhimu akiokoa penati moja huku Willian, Azpilicueta, David Luiz, Kante na Eden Hazard wakifunga penati zote na kufanya Chelsea tupite kwa ushindi wa matuta 5-3.
Turudi kwenye habari kuu, mara baada ya mchezo huo kocha Antonio Conte hakusita kuelezea lawama zake akiilalamikia kadi nyekundu aliyopewa Alvaro Morata akidai haikupaswa kuwa kadi nyekundu ambapo nyota huyo alipewa kadi mbili za njano zilizomaanisha kuwa kadi nyekundu.
"Kama kweli alijiangusha basi ni kweli ilistahili kupewa kadi ya njano, lakini sitaki kulalama sana kwa maana kuna huu mfumo (VAR-Mwamuzi msaidi wa video). Kama mtu akipigwa ngumi au kiwiko inatakiwa pia iwe makini kuonyesha. Sikufurahishwa na kadi ya pili ya njano aliyopewa Morata. Ile ya kwanza huenda ilikuwa kweli. Katika michezo kama hii inabidi utulie na kuwa na umakini mkubwa ili uwe na maamuzi sahihi" alisema kocha Antonio Conte
Mara baada ya mchezo huo kumekuwa na malalamiko mengi juu ya mfumo huo wa VAR unavyofanya kazi ambao wenyewe huwa ni kama kumsaidia mwamuzi afanye mahamuzi sahihi pale anapokuwa anahisi hana maamuzi sahihi ambapo anawasiliana na waamuzi wengine waliopo kwenye chumba kilicho na huo mfumo na wao ndio wanampa majibu sahihi.
CONTE AMTETEA MORATA, CHELSEA IKISHINDA IKIWA PUNGUFU
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment