Kumezuka fununu za chini kwa chini zikieleza kuwa baadhi ya wachezaji wa Chelsea wamekuwa hawana furaha chini ya kocha Antonio Conte haswa kukielezwa kisa kikiwa mgogoro uliokuwa kati ya kocha na nyota wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anaichezea Atletico Madrid, Diego Costa.
Kocha Antonio Conte ameeleza kuwa yeye hajali mchezaji kuwa na furaha ama laah na badala yake anajali kwanza faida na malengo ya timu yatimizwe kwanza kisha maslahi au hisia za mchezaji zije baadae.
"Sipo kwa ajili ya kutimiza au kumfanya mchezaji flani awe nafuraha, ningekuwa na nia iyo basi leo timu ingekuwa ipo kwenye nafasi za mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu"
"Muda mwengine ata ukimfanya mchezaji asiwe na furaha kwa manufaa ya klabu baadae atakuja kukuelewa nayeye mwenyewe ataelewa"
"Nimepita chini ya makocha wengi pindi nikiwa nacheza mpira na ata baada ya kucheza, na wote hakuna aliyewai kunifundisha kuwa muhimu ni kujali kama mchezaji ana furaha ama vipi. Najaribu kuweka malengo ya klabu au timu mbele kisha mchezaji anafata" alisema kocha Antonio Conte.
No comments:
Post a Comment