Klabu ya Everton imetolewa nje kwenye jitihada zake za kumsajili mlinzi wa kushoto wa Chelsea, Baba Rahman ambaye ni raia wa Ghana.
Everton imetajwa kumfukuzia nyota huyo ambaye anatajwa kutaka kurudi klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani aliyoenda kuichezea kwa mkopo msimu uliopita kabla ya kupata majeraha mabaya yaliyomweka nje msimu mzima na sasa klabu hiyo inatajwa kumtaka nyota huyo aungane tena na klabu hiyo.
Baba Rahman alirudi Chelsea kufanyiwa matibabu na sasa anatajwa kuanza mazoezi na inaonekana yupo imara kurejea uwanjani.
No comments:
Post a Comment