HAZARD NA WILLIAN WAMKOSOA CONTE - Darajani 1905

HAZARD NA WILLIAN WAMKOSOA CONTE

Share This

Mara baada ya mchezo wa jana ambao ndio ulikuwa ushindi wa kwanza kwa Chelsea mara baada ya kuwepo mfululizo wa matokeo ya kusuluhu ikiibamiza Brighton iliyokuwa nyumbani magoli 4-0 huku Eden Hazard akiibuka kuwa nyota wa mchezo. Nyota huyo alifanyiwa mahojiano akiwa pamoja na nyota mwenzake, Willian ambaye naye alicheza vizuri mchezo wa ligi kuu.

Walipofanyiwa mahojiano, nyota hao walimkosoa kocha Antonio Conte kwa kutumia mfumo wa 3-5-2 ambao unamfanya Hazard aanze pamoja na Morata katika nafasi ya ushambuliaji na kumuacha Willian nje huku akiingia kama mchezaji wa akiba, wakati unapotumika mfumo wa 3-4-3 unawafanya Willian na Hazard wacheze pamoja ambapo kwa mfumo huo ulitumika hiyo jana na kuifanya Chelsea ipate ushindi huo muhimu. Huku ikicheza pamoja na Michy Batshuayi.

Hazard; Nadhani kocha anaelewa
Willian; kuwa tunacheza vizuri tukiwa pamoja
(Wote wanacheka)

***Je una maoni gani katika hili? unadhani Chelsea inapaswa kutumia mfumo upi, 3-5-2 au 3-4-3?

No comments:

Post a Comment