HERI YA KUZALIWA MOURINHO - Darajani 1905

HERI YA KUZALIWA MOURINHO

Share This

Inabidi tumtakie heri ya kuzaliwa japo kwetu tunamuona kama msaliti kwa kwenda kuifundisha timu ambayo hakuna shabiki wa Chelsea anaipenda, Manyumbu (Man utd).

Kabla sijaanza kukwambia kwanini nimesema msaliti, nataka nikukumbushe kauli aliyowai kuisema moja kati ya makocha bora duniani, Carlo Ancellotti ambaye alishawai kuifundisha Chelsea. Alisema "Mimi leo nimeshaifundisha Real Madrid, siwezi kwenda kuifundisha tena Barcelona" alimaanisha sio vyema kutoka klabu moja na kwenda kufundisha klabu nyengine ambayo unajua kabisa kuwa ni wapinzani wako.

Ila mwisho wa siku soka sio vita ndio maana leo nimeamua kumtakia heri.

Mwaka 1963 tarehe kama ya leo alizaliwa raia huyu wa Ureno ambapo mwisho aliamua kuingia kwenye ukocha mara baada ya kuona hana mwendelezo mzuri kwenye uchezaji wa mchezo huo.

Alikuwa kocha msaidizi kwa klabu kadhaa kabla ya baadae kukabidhiwa klabu ya Benfica ambayo hakuifundisha sana na baadae akaenda kwenye klabu moja ndogo, kisha akaibuka FC Porto na baadae kutua Darajani ambapo hapo alifika mwaka 2004, muda mfupi baada ya tajiri wa kirusi, Roman Abramovich kuinunua Chelsea.

Akaipatia Chelsea mataji mawili huku akitengeneza umaarufu wa hali ya juu huku akinogeshwa na kushangilia kwake.

Baada ya miaka mingi leo Mourinho yupo kwenye klabu ambayo naamini hakuna shabiki wa Chelsea anayeipenda, yupo Manyumbu (Man utd).

Heri ya kuzaliwa kwako Mourinho.

No comments:

Post a Comment