Nyota wa zamani ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka, Tony Giles amemtetea kocha wa Chelsea, Antonio Conte juu ya kubebeshwa mzigo juu ya matokeo mabovu iliyokuwa nao msimu huu na huku ikionekana ni kama Chelsea imeshindwa kutetea taji lake akisema matatizo yote hayo yamesababishwa na bodi ya Chelsea kwa kushindwa kumthamini kocha huyo kwa kumletea wachezaji ambao kocha hajaridhika nao.
"Waangalie United walichokifanya kwa kumpata mchezaji mwenye hadhi kubwa kama Alexis Sanchez huku wakiwapiku majirani zao ambao pia wanagombania nao ubingwa"
"City watajutia kwa kushindwa kumnasa nyota huyo, na kama Pep Guardiola atakuwa ameumizwa kwa nyota huyo kwenda United ambapo huko ataweza kuifikisha ikawa sehemu nzuri, jiulize anajisikiaje kocha wa mabingwa watetezi, Antonio Conte?"
"Conte anavyofanyiwa pale Stamford Bridge sio haki kabisa ni kama kuonewa na haionekani kama itakuwa na mwisho. Mourinho amefanikiwa kuwanasa Nemanja Matic na Alexis Sanchez ambao wote ni bora, lakini Conte anapelekewa wachezaji kama Andy Carroll na Peter Crouch, kweli ni haki?"
"Kwa hali hiyo naona itakuwa ngumu sana kwa Chelsea kuutwaa tena ubingwa kama itaendelea kufanya inachokifanya" alisema gwiji huyo.
Je una maoni gani katika hili? unadhani alichokiongea ni kweli?
Toa maoni yako hapo chini
No comments:
Post a Comment