KOCHA CONTE AELEZEA USAJILI KUELEKEA KUFUNGWA KWA DIRISHA - Darajani 1905

KOCHA CONTE AELEZEA USAJILI KUELEKEA KUFUNGWA KWA DIRISHA

Share This
Kesho Chelsea itakuwa uwanjani kumenyana dhidi ya Afc Bournemouth, katika mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa mchezo wa 25, lakini pia kesho hiyohiyo dirisha la usajili la mwezi huu wa januari litakuwa linafungwa na Chelsea itakuwa ni mojawapo ya klabu ambazo zitakuwa zimenufaika au kutokunufaika kutokana na usajili ilioufanya uwe kama umetibu kidonda au laah.

Lakini kuelekea kwenye mchezo huo, kocha wa Chelsea, Antonio Conte amefanya mkutano na waandishi wa habari akiulizwa mambo yanayoendelea klabuni hapo, na kati ya mambo aliyoulizwa ameulizwa pia juu ya usajili ambao Chelsea imehusishwa nao katika dirisha hili la usajili.

"Nina matumaini na kila jambo muhimu lakini kizuri zaidi ni kuwa na matumaini na uhalisia. Na uhalisia wenyewe ni huu, natakiwa kuandaa timu kwa ajili ya mchezo wa kesho katika usahihi na kama inavyotakiwa nami nina furaha katika hilo" alisema kocha huyo.

Na alipoulizwa juu ya Chelsea kumtaka mshambuliaji wa As Roma, Edin Dzeko, kocha huyo alijibu "Nadhani huyo ni mchezaji halali wa Roma na nafikiri ataendelea kuwa mchezaji wa klabu hiyo"

Na alipoulizwa juu ya Chelsea kuhusishwa na mshambuliaji wa Arsenyani (Arsenal), Olivier Giroud, kocha Antonio Conte alijibu "Majukumu yangu ni kuiambia klabu nahitaji wachezaji gani na klabu inajaribu kadri inavyoweza kutimiza hilo. Mi kazi yangu ni kuwaambia nawahitaji wachezaji wa nafasi gani na wa aina gani, kisha wao ndio wanajaribu kutimiza"

Na alipoulizwa juu ya Chelsea kumtaka mshambuliaji raia wa Hispania, Fernando Llorente ambaye anaichezea klabu ya Tottenham, kocha huyo alijibu "Kipindi cha kiangazi kilikuwa ni kipindi cha kiangazi, na mwezi huu wa Januari ni kipindi cha baridi. Ni maswala mawili tofauti ambayo kamwe hayafanani. Tunaongelea maswala juu ya wachezaji wa klabu nyengine (Kocha Antonio Conte huwa hapendi kuzungumzia wachezaji wengine, ndio maana nafikiri hapa amejibu hivyo kuonyesha kuwa hataki maswali juu ya wachezaji wengine yaendelee)"

Kuhusu kujibu kuwa kipindi cha kiangazi hakifanani na kipindi hiki, kama Darajani 1905 tunafikiri alitaka kuwaambia kuwa kwa sasa Chelsea haimhitaji mchezaji huyo ingawa iliwai kuhusishwa kumtaka katika kipindi cha dirisha kubwa la usajili la kipindi cha kiangazi ila kwa sasa hayupo kwenye mipango ya timu.

No comments:

Post a Comment