Mara baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Celtic ya nchini Scotland, Charly Musonda Jr ambaye ni raia wa Ubelgiji anadaiwa kuipotezea kabisa klabu yake ya Chelsea ambayo ametokea kabla ya kujiunga na klabu hiyo inayopatikana jiji la Glasgrow nchini humo.
Kupitia vyanzo kadhaa inaelezwa kuwa nyota huyo ameacha kuwafatilia (unfollow) wachezaji karibu wote wa Chelsea kupitia mtandao wa Instagram huku anaoendelea kuwafatilia mpaka sasa ni Antonio Rudiger, Gary Cahill, Alvaro Morata pamoja na mkongwe wa Chelsea, John Terry huku pia akiacha kuifatilia Chelsea katika mtandao wa Twitter.
Lakini pia chanzo hicho kinadai kuwa nyota huyo ameacha kumfatilia nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye mara kadhaa aliwai kukaririwa kuwa ni mmoja ya wachezaji anaowapenda na kuwafatilia kwa karibu, lakini pia chanzo hicho kinadai nyota huyo amewafatilia kwa wingi na wachezaji wa klabu yake mpya ya Celtic ambapo yupo hapo kwa mkataba wa miezi 18.
Lakini Darajani 1905 inaelewa kuwa huenda hii imetokea kutokana na nyota huyo mwenye miaka 21 kukasirishwa mara baada ya kutopendezwa na maamuzi ya Chelsea juu ya usajili wake mara baada ya kuwai kuripotiwa kuwa nyota huyo alitaka kujiunga na klabu ya Real Betis ambayo aliwai kuichezea kwa mkopo kabla ya kurejea tena Chelsea mwezi januari mwaka jana.
Katika dirisha hili la usajili klabu hiyo ilidai kumtaka tena nyota huyo naye alipendelea kuungana na klabu hiyo ingawa Chelsea haikutaka kumpeleka kwenye klabu hiyo ianyopatikana nchini Hispania ambapo kuna taarifa zililipoti kuwa Chelsea inataka nyota huyo ajiunge na klabu ya nchi ambazo zinacheza soka la kufanania na soka la Uingereza.
MUSONDA HATAKI KUSIKIA KITU KUTOKA CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
# Mitandaoni
Share This
About Darajani 1905
Mitandaoni
Labels:
Chelsea Habari,
Mitandaoni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment