Ni usiku mwengine mbovu na mgumu kwa kila shabiki wa Chelsea duniani kote, huku Morata akitukosesha ushindi muhimu mara baada ya kukosa nafasi tatu za wazi ambazo angeweza kufunga kirahisi.
Mchezo ulikuwa wa kupokezana kushambuliana ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinaisha, bado hakuna aliyefanikiwa kuliona goli la mwenzake na matokeo kuwa 0-0 huku Morata akikosa nafasi ya wazi kabisa ambayo ingeweza kuifanya Chelsea iongoze.
Chelsea ilianza kufungwa goli la kwanza kupitia kwa Wilshere akifunga kwa shuti kali na Arsenyani(Arsenal) kuwa mbele kwa goli 1-0.
Dakika kadhaa baadae, Chelsea ilipata penati ambapo Eden Hazard alichezewa madhambi katika eneo la hatari na penati hiyo kupigwa nayeye mwenyewe na kufunga kisha kufanya matokeo kuwa 1-1.
Lakini kocha Antonio Conte akaamua kufanya mabadiliko akiwatoa Eden Hazard na kumwingiza Willian Borges huku pia akimtoa Victor Moses na kumwingiza Davide Zappacosta na Fabregas nafasi yake ikichukuliwa na Danny Drinkwater.
Na mabadiliko hayo yalikuwa na faida mara baada ya Willian kutengeneza shambulizi kwa kutoa pasi ndefu iliyomfikia Zappacosta na baadae kutoa pasi katika eneo la hatari na Marcos Alonso akafunga goli safi kabisa na kuifanya Chelsea iwe mbele kwa bao 2-1.
Lakini dakika kadhaa baadae wakati mpira ukielekea kuisha Arsenyani wakachomoa goli kupitia kwa Bellerin na kufanya matokeo kuwa 2-2.
Kwa matokeo hayo yanaifanya Chelsea iendelee kusalia nafasi ya tatu ikiwa na alam 46 huku ikiachwa alama moja na Manyumbu (Man utd) inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 47 na Mama site(Man city) ikiwa kileleni ikiiacha Chelsea kwa alama 16 ambapo wao wana alama 62.
*****Kama mashabiki wa Chelsea tunasema leo tumeangushwa na Alvaro Morata akikosa kufunga nafasi za wazi kabisa, yeye ndio alikuwa mtu wa kuifanya Chelsea leo iondoke na alama tatu za muhimu.
No comments:
Post a Comment