UMEUSIKIA UTABIRI WALIOUFANYA KWA CHELSEA? - Darajani 1905

UMEUSIKIA UTABIRI WALIOUFANYA KWA CHELSEA?

Share This
Hapa nimekuletea maoni ya wachambuzi wanaofanya kazi kwenye chombo cha habari za michezo cha Skysports. Wametoa maoni juu ya ligi kuu Uingereza itakavyokuja kuisha na msimamo utakavyokuwa kwenye klabu sita za juu.

Paul Merson [Mchezaji wa zamani wa Arsenyani (Arsenal)]
1. Manchester City
2. Manchester United
3. Tottenham
4. Liverpool
5. Chelsea
6. Arsenal
"Kwa mara ya kwanza nimekuwa na wasiwasi na Chelsea, wamekuwa hawafungi magoli. Michy Batshuayi anaonekana kuondoka klabuni hapo kwa maana hiyo watabaki na mshambuliaji mmoja, Alvaro Morata. Na kwa kuwa peke yake maana yake watakuwa na mtu aliyechoka kutokana na kushiriki michuano mingi"
"Kumekuwa na maswali mengi juu ya wapi ataenda Sanchez, kama ataenda Chelsea basi watamaliza katika timu nne za juu hiyo halina ubishi"
Phil Thompson [Mchezaji wa zamani wa Liverpumba (Liverpool)]
1. Manchester City
2. Liverpool
3. Manchester United
4. Chelsea
5. Tottenham
6. Arsenal
"Naona kuna upinzani mkubwa katika kugombea nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya kati ya Chelsea na Tottenham. Kwa upande wa Tottenham wamekuwa na mfululizo ambao hauna uhakika, kwa maana hiyo karata yangu naiweka kwa Chelsea"
Charlie Nicholas [Mchezaji wa zamani wa Arsenyani (Arsenal)]
1. Manchester City
2. Liverpool
3. Manchester United
4. Tottenham
5. Chelsea
6. Arsenal
"Tottenham wamekuwa na mfululizo mzuri katika ufungaji wakati Chelsea wanaonekana kutokuwa na wingi wa magoli, namuona Conte akiangaika kutatua tatizo hili katika dirisha hili la usajili"
Matt Le Tissier [Mchezaji wa zamani wa Southampton]
1. Manchester City
2. Manchester United
3. Tottenham
4. Liverpool
5.Chelsea
6. Arsenal
"Siioni Chelsea ikiwa na ubora huo, Alvaro Morata hana moto tena wakati Eden Hazard akionekana kushuka kiwango na hapohapo kuna wasiwasi juu ya nafasi ya kocha ikionekana bado kutokuwa na majibu kamili."
***Lakini sioni tatizo katika hili, hizi zote zinabaki kuwa fikra zao na mawazo yao, hawahawa wachambuzi walimtabiria Antonio Conte kumaliza nje ya nne bora msimu uliopita ila akaja kuwa bingwa. Muhimu ni kupambana na kushindania mataji yale tunayoshiriki.

No comments:

Post a Comment